Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 2:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni maadui za kila mtu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni maadui za kila mtu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni maadui za kila mtu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 wale waliomuua Bwana Isa na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 wale waliomuua Bwana Isa na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote,

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 2:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali!


Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.


Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.


na jinsi makuhani wakuu na wakubwa wetu walivyomtoa kwa hukumu ya kufa, wakamsulibisha;


Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamtwaa na Petro. Siku hizo ndizo siku za mikate isiyochachwa.


mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambae ninyi mlimwua mkamtundika katika mti.


Ni yupi katika manabii ambae baba zenu hawakumwudhi? nao waliwaua wale waliotabiri khabari za kuja kwake yule mwenye haki; ambae ninyi sasa mmemsaliti mkamwua;


Lakini walio wengi, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.


kwa kusafiri marra nyingi; khatari za mito; khatari za wanyangʼanyi; khatari kwa jamaa; khatari kwa mataifa; khatari za mijini; khatari za jangwani; khatari za baharini; khatari kwa ndugu za uwongo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo