Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: Tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, nyinyi mliusikia, mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu nyinyi mnaoamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: Tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, nyinyi mliusikia, mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu nyinyi mnaoamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, nyinyi mliusikia, mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu nyinyi mnaoamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, linalotenda kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 2:13
41 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Baba yenu asemae ndani yenu.


Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma.


Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika.


IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti:


Na mfano ndio huu: Mbegu ni neno la Mungu.


Lakini yeye akajibu akawaambia, Mama yangu na ndugu zangu ndio hawa walisikialo neno la Mungu na kulitenda.


Ninyi mmekwisba kuwa safi kwa sababu ya neno nililowaambia.


Uwatakase kwa kweli; neno lako ndio kweli.


Na kwa ajili yao najitakasa, illi na hawa watakaswe katika kweli.


Marra nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Bassi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu.


Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.


Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.


Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu.


Na mitume walioko Yerusalemi, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana.


Bassi imani, chanzo chake ni kusikla; na kusikia kunakuja kwa neno la Mungu.


Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.


na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Maana ni kweli, sisi nasi tumekhubiriwa khabari njema kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa bao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Bali Neno la Bwana hudumu hatta milele. Na neno bilo ni neno lile jema lililokhubiriwa kwenu.


kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;


mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.


Na killa mwenye kunitumainia hivi hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo