Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 2:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 vile vile kama mjuavyo jinsi tulivyomwonya killa mmoja wemi kama baba amwonavyo mtoto wake, tukiwatieni moyo na kushuhudia,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe. Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe. Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe. Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Maana mnajua kwamba tuliwatendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Maana mnajua kwamba tuliwatendea kila mmoja wenu kama vile baba awatendeavyo watoto wake.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 2:11
40 Marejeleo ya Msalaba  

maana nina ndugu watano; awashuhudie, wasije nao mahali hapa pa adhabu.


Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


bali tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.


ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


Bassi, farijianeni mkajengeane, killa mtu mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo?


Bassi twawaagiza, hao na kuwaonya katika Bwana wetu Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.


Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.


Uwaagize haya, illi wawe bawana lawama.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha;


Na wale walio na mabwana waaminio, wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; hali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya kazi zao wamekuwa wenye imani na kupendwa. Uwafundishe mambo haya, na kuonya.


Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.


Na vijana vivyo hivyo nwaonye kuwa na kiasi;


Watumwa wawatii Bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,


Nawasihini, ndugu, livumilieni neno hili lenye maonyo; maana nimewaandikia kwa maneno machache.


Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo