Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 2:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 2:10
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa.


Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote,


Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina khatiya kwa damu ya mtu aliye yote.


Nami ninajizoeza katika neno hili kuwa na dhamiri isiyo na khatiya mbele ya Mungu na mbele ya watu.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Kwa nini? kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.


Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliye mtukufu hatta milele, ajua va kuwa sisemi nwongo.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia.


Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu, hatukumharibu mtu, hatukumkalamkia mtu.


kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.


Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya kuficha tamaa; Muugu ni shahidi.


Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata, kwa sababu hatukwenda bila utaratibu kwenu;


Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu.


Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,


wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya mfano kwa lile kundi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo