Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 1:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, yaani Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, yaani Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, yaani Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani Isa, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mwenyezi Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Isa, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 1:10
46 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao.


Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?


Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Bassi akawaambia makutano waliotokea illi kubatizwa nae, Enyi uzao wa nyoka, ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu itakayokuja?


wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.


Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


hatta hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;


Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:


Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbiuguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu Kristo;


Nae ni kichwa cha mwili, yaani cha kanisa; nae ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, illi awe mtangulizi katika yote.


hatta mkawa mfano kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.


wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.


bali tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.


Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


bali kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


mkitazamia hatta ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo