Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kundi la waumini la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu, Baba yetu, na ndani ya Bwana wetu Isa Al-Masihi. Neema iwe kwenu na amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kundi la waumini la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu, na ndani ya Bwana Isa Al-Masihi: Neema iwe kwenu na amani.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 1:1
30 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Bassi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambieni maneno yayo hayo kwa vinywa vyao.


Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.


Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji;


Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza.


Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila;


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.


Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo.


Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia.


kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako.


na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia,


Lakini sikujulika uso wangu na makanisa ya Yahudi yaliyo katika Kristo;


Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwaua Yesu Kristo.


PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,


PAOLO, Silwano, na Timotheo kwa kanisa la Wathessaloniki lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo:


kwa Timotheo, mwana wangu khassa katika imani, Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; pamoja nae nitawaoneni, kama akija upesi.


Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo