Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 9:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Je! ninanena haya kama mwana Adamu? Au sharia nayo haisemi yayo hayo?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, sheria nayo haisemi hivyo?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, sheria nayo haisemi hivyo?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, sheria nayo haisemi hivyo?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Je, nasema mambo haya katika mtazamo wa kibinadamu tu? Je, Torati haisemi vivyo hivyo?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Je, nasema mambo haya katika mtazamo wa kibinadamu tu? Je, Torati haisemi vivyo hivyo?

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 9:8
9 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, je! twaibatilisha sharia kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithubutisha sharia.


Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)


Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.


Wanawake wanyamaze katika kanisa, maana hawana rukhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo sharia nayo.


Lakini yu kheri zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi; nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho ya Bwana.


Kwa maana injili biyo niliyowakhubiri nawajulisha, ndugu, ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.


Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.


Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo