Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 9:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano ili mkapata tuzo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 9:24
18 Marejeleo ya Msalaba  

Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki.


Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula sehemu ya vitu vya hekalu, na wale waikhudumiao madhbahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhbahu?


Nami nafanya haya yote kwa ajili ya Injili nipate kuishiriki pamoja na wengine.


Hatta mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitae; napigana vivyo hivyo, si kama apigae hewa:


Nami nalikwenda kwa kufunuliwa, nikawaeleza injili ile niikhubirivyo katika mataifa, lakini kwa faraglia kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio burre au nalipiga mbio burre.


Mlikuwa mkipiga mbio vizuri: ni nani aliyewazuia msiitii kweli?


nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre.


Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali nafuatafuata illi nilishike lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.


nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.


Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake,


BASSI na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, tuweke kando killa mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa uvumilivu katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo