Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 9:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Bassi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nikhubiripo, nitatoa Injili ya Kristo bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu haki yangu niliyo nayo katika Injili.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Basi je, thawabu yangu ni nini? Thawabu yangu ni hii: Ya kwamba katika kuhubiri Injili niitoe bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Basi je, thawabu yangu ni nini? Thawabu yangu ni hii: Ya kwamba katika kuhubiri Injili niitoe bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.

Tazama sura Nakili

1 Wakorintho 9:18
16 Marejeleo ya Msalaba  

Avunae hupokea mshahara na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, illi yeye apandae na yeye avunae wafurahi pamoja.

Akafika kwao; na kwa kuwa kazi yake na kazi yao ni moja, akakaa kwao, akafanya kazi yake, kwa maana walikuwa mafundi wa kufanyiza khema.

Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambae Kristo alikufa kwa ajili yake.

vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, bali faida yao walio wengi, wapafe kuokolewa.

Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.

Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.

Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaze wale walio dhaifu.

Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.

Lakini sikutumia mambo haya hatta moja. Wala sikuvaandika haya illi iwe hivyo kwangu; maana ni kheri nife kuliko mtu aliye vote abatilishe huku kujisihi kwangu.

Maana nikiitenda kazi hii kwa khiari yangu nina thawabu; kama si kwa khiari yangu, illakini nimeaminiwa uwakili.

Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.

Hatukutaka kusifiwa na watia Adamu, wala na ninyi, wala na wengine, tulipokuwa tuliweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo