Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 9:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo. Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo. Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo. Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi? Lakini sisi hatukutumia haki hii. Kinyume chake, tunavumilia kila kitu ili tusije tukazuia Injili ya Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi? Lakini sisi hatukutumia haki hii. Kinyume chake, tunavumilia kila kitu ili tusije tukazuia Injili ya Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

1 Wakorintho 9:12
23 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu, enyi wana sharia, kwa sababu mliuchukua ufunguo wa maarifa; ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mliwazuia.

Akafika kwao; na kwa kuwa kazi yake na kazi yao ni moja, akakaa kwao, akafanya kazi yake, kwa maana walikuwa mafundi wa kufanyiza khema.

Ndio sababu nalizuiwa marra nyingi nisije kwenu.

hustahimili yote, huamini yote, hutumaini yote, huvumilia yote.

Bassi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyangʼanywa mali zenu?

Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waikhubirio Injili wamzukiwe kwa Injili.

Lakini sikutumia mambo haya hatta moja. Wala sikuvaandika haya illi iwe hivyo kwangu; maana ni kheri nife kuliko mtu aliye vote abatilishe huku kujisihi kwangu.

Maana, ijapokuwa naikhubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimepewa sharti; tena ole wangu nisipoikhubiri.

Bassi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nikhubiripo, nitatoa Injili ya Kristo bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu haki yangu niliyo nayo katika Injili.

Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, illakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana muhuri ya utume wangu ni ninyi katika Bwana.

Lakini nifanyalo nitalifunya, illi niwapinge watafutao nafasi wasipate nafasi; illi katika neno hilo wajisifulo waonekane kuwa kama sisi.

Maana mwavumilia na mtu akiwatieni utumwani, akiwameza, akiwateka, akijikuza, akiwapiga usoni.

Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,

Tusiwe kwao la namna yo yote katika jambo lo lote, khuduma yetu isilaumiwe;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo