Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 9:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 JE! mimi si mtume? mimi si huru? sikumwona Yesu Kristo Bwana wetu? ninyi si kazi yangu katika Bwana?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, nyinyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, nyinyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, nyinyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Isa, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Isa, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana Isa?

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 9:1
37 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia.


Walakini mitume Barnaba na Paolo, walipopata khabari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina hwana, mbona mnafanya haya?


Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume.


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Saul, Bwana amenipeleka, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.


Hatta alipokuwa akisafiri akawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza nuru kutoka mbinguni.


Akasema, U nani Bwana? Akasema, Mimi ndimi Yesu unaeniudhi wewe.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu.


PAOLO, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,


Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?


Na nikitumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho?


Lakini mtu aliye yote, akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.


Mimi nilipanda, Apollo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.


Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, illi nipate watu wengi zaidi.


Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.


Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa kitu walicho nacho mitume walio wakuu.


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Hatukutaka kusifiwa na watia Adamu, wala na ninyi, wala na wengine, tulipokuwa tuliweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo