Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 8:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaze wale walio dhaifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini, jihadharini: Huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini, jihadharini: Huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini angalieni jinsi mnavyotumia uhuru wenu usije ukawa kikwazo kwao walio dhaifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini angalieni jinsi mnavyotumia uhuru wenu usije ukawa kikwazo kwao walio dhaifu.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 8:9
27 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu.


Mtu asitafute kujifaidia nafsi yake, bali kumfaidia mwenzake.


Lakini mtu akiwaambieni, Kitu hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu, msile, kwa ajili yake yeye aliyekuonyesha, na kwa ajili ya dhamiri; maana dunia ni mali ya Bwana na vitu vyote viijazavyo.


Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?


Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunaui wala Kanisa la Mungu:


Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na elimu, umeketi chakulani ndani ya hekalu ya sanamu, je! dhamiri yake mtu huyu, kwa kuwa yu dhaifu, haitathubutika hatta ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?


Na hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuwajeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo.


Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, illi niwapate wanyonge. Nalikuwa mtu wa hali zote kwa watu wote, illi nipate kuwaokoa watu kwa njia zote.


Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Illakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), na mimi niuao ujasiri.


Nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu na mimi? Nani aliyechukizwa na mimi nisiwake?


Tusiwe kwao la namna yo yote katika jambo lo lote, khuduma yetu isilaumiwe;


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.


Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu.


wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule.


Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo