Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 6:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mwenyezi Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti,

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 6:9
51 Marejeleo ya Msalaba  

Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena.


Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao.


Msidanganyike: mazumgumzo mabaya huharibu tabia njema.


Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.


Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu?


YAKINI khabari imeenea ya kama kwenu kuna zina, na zina hiyo ya namna isiyonenwa hatta katika mataifa, kwamba mtu awe na mke wa baba yake.


Sisemi msichangamane kabisa kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani an wanyangʼanyi, an wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.


Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.


wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi.


Ikimbieni zina. Killa dhambi aifanyayo mwana Adamu ni nje ya mwili wake; bali yeye afanyae zina hufanya dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.


Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;


Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.


nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.


Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


Asiwepo asharati au asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.


Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.


Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi.


Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo