Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 6:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Bassi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaha? Hasha!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya mwili wa Kristo? Je, mnadhani naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa sehemu ya mwili wa kahaba? Hata kidogo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya mwili wa Kristo? Je, mnadhani naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa sehemu ya mwili wa kahaba? Hata kidogo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya mwili wa Kristo? Je, mnadhani naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa sehemu ya mwili wa kahaba? Hata kidogo!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Al-Masihi mwenyewe? Je, nichukue viungo vya mwili wa Al-Masihi na kuviunganisha na mwili wa kahaba? La hasha!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Al-Masihi mwenyewe? Je, nichukue viungo vya mwili wa Al-Masihi na kuviunganisha na mwili wa kahaba? La hasha!

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 6:15
25 Marejeleo ya Msalaba  

Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.


vivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na sisi sote tu viungo killa mmoja kwa wenzake.


Bassi, je! twaibatilisha sharia kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithubutisha sharia.


Hasha! kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?


Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha!


Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?


Bassi je! Ile iliyo njema ilikuwa manti kwangu mimi? Hasha! hali dhambi, illi ionekane kuwa dhambi, ilinifanyizia mauti kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.


Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.


Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha killa mwanamume ni Kristo na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.


Na ninyi m mwili wa Kristo, na viungo vya mwili huo, mmoja hiki na mmoja hiki.


Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu ataharibu vyote viwili, tumbo na vyakula. Na mwili si kwa zina, hali ni kwa Bwana, nae Bwana ni kwa mwili.


Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja nae.


Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;


Hamjui ya kuwa tutawahukumu malaika, bassi si zaidi sana mambo ya maisha haya?


Lakini kama sisi wenyewe tulipokuwa tukitafuta kufanyiziwa wema katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha.


Bassi, torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha. Kwa kuwa, kama ingalitolewa sharia iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sharia.


Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


Maana mume ni kichwa cha mke, kama nae Kristo ni kichwa cha kanisa; nae ni mwokozi wa mwili.


kwa kuwa tu viungo vya mwili wake, na nyama yake, na mifupa yake.


wala hakishiki kiehwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua mkuo utokao kwa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo