Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 6:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywa watakatifu, na kufanywa waadilifu na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywa watakatifu, na kufanywa waadilifu na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywa watakatifu, na kufanywa waadilifu na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Isa Al-Masihi na katika Roho wa Mungu wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Isa Al-Masihi na katika Roho wa Mwenyezi Mungu wetu.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 6:11
52 Marejeleo ya Msalaba  

na hawo nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo liaki nitakupeni. Wakaenda.


Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Yesu akamwambia, Aliyekwisha kuoga hana haja illa ya kunawa miguu, hali yu safi mwili wote; na ninyi m safi, lakini si nyote.


Petro akamwambia. Hutanitawadha miguu milele. Yesu akamwambia, Nisipokutawadha, huna fungu pamoja nami.


Kwa maana kuna wakati malaika hushuka akaiingia ile birika, akayatibua maji: bassi yeye aliyeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, akaponea ugonjwa wote uliokuwa umempata.


na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa.


Bassi sasa, unakawiliani? Simama ubatizwe ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


wanapewa haki burre kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Yesu Kristo:


Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Bassi zaidi sana tukiisha kupewa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza.


Ni nani atakaewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye awahesabiae haki.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Mwajua ya kuwa mlipokuwa Mataifa mlichukuliwa kwa sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Ni dhahiri ya kwamba hapana mtu ahesabiwae kuwa ana haki nibele za Mungu katika sharia; kwa sababu Mwenye haki ataisbi kwa imani.


Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani.


Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


Kwa maana zamani mlikuwa giza, bali sasa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru;


Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo