Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 5:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 YAKINI khabari imeenea ya kama kwenu kuna zina, na zina hiyo ya namna isiyonenwa hatta katika mataifa, kwamba mtu awe na mke wa baba yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Yamkini habari imeenea ya kuwa miongoni mwenu kuna uzinzi ambao haujafanyika hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu: Kwamba mtu anaishi na mke wa baba yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Yamkini habari imeenea ya kuwa miongoni mwenu kuna uzinzi ambao haujatokea hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu: Kwamba mtu anaishi na mke wa baba yake.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 5:1
32 Marejeleo ya Msalaba  

balituwaandikie wajiepushe na unajisi wa sanamu na asharati na nyama zilizosongwa na damu.


mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.


Kwa maana nimearifiwa khabari zenu, ndugu, na wale walio wa nyumba ya Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.


Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.


Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu ataharibu vyote viwili, tumbo na vyakula. Na mwili si kwa zina, hali ni kwa Bwana, nae Bwana ni kwa mwili.


Ikimbieni zina. Killa dhambi aifanyayo mwana Adamu ni nje ya mwili wake; bali yeye afanyae zina hufanya dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira,


nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.


Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi, bali kwa sehemu ninyi nyote, nisije nikawalemea.


Bassi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake aliyedhulumiwa, bali ijtihadi yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.


Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki,


Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu;


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.


Nami nimempa muda illi atubu uzinzi wake, nae bataki kutubu.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo