Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 4:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Maana ni nani anaekupambanua na mwingine? na una, nini usiyoipokea? Na iwapo uliipokea, wajisifiani kana kwamba hukuipokea?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kwa maana ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na wengine? Ni nini mlicho nacho ambacho hamkupokea? Nanyi kama mlipokea, kwa nini mnajivuna kama vile hamkupokea?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kwa maana ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na wengine? Ni nini mlicho nacho ambacho hamkupokea? Nanyi kama mlipokea, kwa nini mnajivuna kama vile hamkupokea?

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 4:7
29 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaita watu kumi katika watumishi wake, akawapa mane za fedha kumi, akawaambia, Fanyeni biashara hatta nitakaporudi.


Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.


Bassi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;


Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?


Maana nipendalo ni watu wote wawe kama mimi nilivyo; illakini killa mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo