Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 4:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Lakini nitakuja kwemi upesi, Bwana akipenda, nami nitajua, si neno lao waliojivuna, bali nguvu zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Lakini kama Bwana Isa akipenda, nitafika kwenu hivi karibuni, nami nitajua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia nguvu yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Lakini kama Bwana Isa akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 4:19
18 Marejeleo ya Msalaba  

bali aliagana nao, akisema. Sina buddi kufanya siku kuu hii inayokuja Yerusalemi: lakini nitarejea kwenu, Mungu akinijalia.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.


nipate kufika kwenu kwa furaha, kama Mungu akipenda, nikapate kupumzika pamoja nanyi.


mtu akiwa na njaa, ale nyumbani; msipate kukutanika kwa hukumu. Nayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.


Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa.


Lakini nitakuja kwenu, nikipita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.


Maana sitaki kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraja kukaa kwenu mda wa kitambo, Bwana akinijalia.


Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;


Wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.


Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.


Lakini mimi namwitia Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijaenda Korintho.


nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu.


Na tutafanya hayo kama Mungu akitujalia.


Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hayi na kufanya hivi au hivi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo