Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 4:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana Isa. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Al-Masihi Isa, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kundi la waumini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana Isa. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Al-Masihi Isa, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kanisa.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 4:17
33 Marejeleo ya Msalaba  

Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.


AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.


Lakini mtu aliye yote, akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


mtu akiwa na njaa, ale nyumbani; msipate kukutanika kwa hukumu. Nayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.


Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.


KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo.


Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:


Siyaandiki haya illi kuwatahayarisha, hali kuwaonya kama watoto niwapendao. Maana ijapokuwa mna waalimu elfu katika Kristo, illakini hamna baba wengi.


Maana mimi ndiye aliyewazaa katika Kristo Yesu kwa Injili.


Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini.


Lakini Mungu alivyomgawia killa mtu—kama Mungu alivyomwita killa mtu, na aenende vivyo hivyo. Na ndivyo ninavyoagiza katika Makanisa yote.


Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana.


Na pamoja nae tukamtuma ndugu yule ambae sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.


Illakini ninyi nanyi mpate kuyajua mamho yangu ni hali gani, Tukiko, ndugu mpendwa, mkhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisha mambo yote;


Walakini natmnaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwemi karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.


Maana mwajua ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku.


Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri;


kwa Timotheo, mwana wangu khassa katika imani, Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.


Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,


Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru;


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo