Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 4:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Maana mimi ndiye aliyewazaa katika Kristo Yesu kwa Injili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hata kama mnao walimu elfu kumi katika Al-Masihi, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Al-Masihi Isa kwa kuwaletea Injili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Hata kama mnao walimu 10,000 katika Al-Masihi, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Al-Masihi Isa kwa kuwaletea Injili.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 4:15
25 Marejeleo ya Msalaba  

kadhalika nikijitahidi kuikhubiri Injili, nisikhubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine,


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama,


Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.


Mimi nilipanda, Apollo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.


Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.


Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.


Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waikhubirio Injili wamzukiwe kwa Injili.


Maana, ijapokuwa naikhubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimepewa sharti; tena ole wangu nisipoikhubiri.


Bassi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nikhubiripo, nitatoa Injili ya Kristo bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu haki yangu niliyo nayo katika Injili.


Nami nafanya haya yote kwa ajili ya Injili nipate kuishiriki pamoja na wengine.


Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.


Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani.


Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini va mwalimu.


Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.


Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti,


kwa Tito, mwanangu katika imani tuishirikiyo: Neema na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu.


Mimi Paoio nimeandika kwa mkouo waugu mweuyewe, nitalipa. Sikuambii kwamba wawiwa nami hatta nafsi yako.


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo