Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 4:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini nyinyi ni wenye busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, nyinyi ni wenye nguvu. Nyinyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini nyinyi ni wenye busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, nyinyi ni wenye nguvu. Nyinyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini nyinyi ni wenye busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, nyinyi ni wenye nguvu. Nyinyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kwa ajili ya Al-Masihi sisi ni wajinga, lakini ninyi mna hekima sana ndani ya Al-Masihi. Sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu. Tunadharauliwa, lakini ninyi mnaheshimiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kwa ajili ya Al-Masihi sisi ni wajinga, lakini ninyi mna hekima sana ndani ya Al-Masihi. Sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu. Tunadharauliwa, lakini ninyi mnaheshimiwa.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 4:10
38 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.


M kheri ninyi watakapowatukana na kuwatesa na kuwanenea killa neno baya kwa uwongo, kwa ajili yangu.


Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.


Yesu akawaambia mfano huu watu waliojidhani nafsi zao kuwa wenye haki, wakiwadharau wengine wote.


M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu.


Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.


Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.


Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa sauti kuu, Paolo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugenza akili zako.


Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wana Adamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wana Adamu.


Bassi anaejidhani amesimama aangalie asianguke.


Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.


Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na khofu na matetemeko mengi.


Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.


Nimewanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa maana mlikuwa hamjakiweza; naam, hatta sasa hamkiwezi, kwa maana hatta sasa m watu wa tabia za mwilini.


Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Na ingekuwa kheri kama mngalimiliki, illi sisi nasi tumiliki pamoja nanyi.


Maana wasema, Nyaraka zake nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini yu dhaifu, na maneno yake hayawi kitu.


Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnavumilia na wajinga kwa furaha.


Nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu na mimi? Nani aliyechukizwa na mimi nisiwake?


Maana twafurahi, sisi tulipo dhaifu, na ninyi hodari. Tena twaomba hili nalo, mtimilike.


Bassi hapo mauti hufanya kazi yake ndani yetu, hali nzima ndani yenu.


kwa utukufu na aibu, kwa kunenwa vibaya na kunenwa vyema; kama wadanganyao, bali watu wa kweli;


Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo