Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 3:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Je, hamjui kwamba ninyi wenyewe ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Je, hamjui ya kwamba ninyi wenyewe ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mwenyezi Mungu anakaa ndani yenu?

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 3:16
24 Marejeleo ya Msalaba  

Roho ya kweli; ambae ulimwengu hauwezi kumkubali, kwa kuwa haumwoni wala haumjui: bali ninyi mnamjua; maana anakaa kwenu, nae atakuwa ndani yenu.


Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki.


Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo, twalibatizwa katika mauti yake?


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


Kama mtu akiiharibu hekalu ya Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu ya Mungu ni takatifu, ambayo ni ninyi.


Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.


Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?


Hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja nae? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.


Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira,


Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula sehemu ya vitu vya hekalu, na wale waikhudumiao madhbahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhbahu?


Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.


Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.


Ilinde ile amana nzuri kwa Rolio Mtakatifu akaae ndani yetu.


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo