Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 2:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Na neno langu na kukhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya kibinadamu yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho zenye nguvu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi, bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 2:4
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


Agrippa akamwambia Paolo, Kwa maneno machache wataka kunifanya kuwa Mkristo.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Maana Kristo hakunituma illi nibatize, bali niikhubiri Injili; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo nsije nkabatilika.


NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.


Nayo twayanena, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali tuliyofimdishwa na Roho, tukiyalinganisha mamho ya rohoni na mambo va rohoni.


Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, hali katika nguvu.


katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki,


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


Nasema neno hili, mtu asije akawadanganyeni kwa maneno yaliyotungwa illi kuwakosesha.


kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.


Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia.


Maana hatukufuata hadithi zilozotungwa kwa werevu, tulipowajulislia ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa mashahidi wa ukuu wake.


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo