Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 16:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Labda nitakaa kwenu; naam, labda nitashinda kwenu wakati wa baridi, mpate kunisafirisha wakati uwao wote nitakapokwenda.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo.

Tazama sura Nakili

1 Wakorintho 16:6
11 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.

Nao walimsindikiza Paolo wakampeleka hatta Athene; na wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kama wasikawie kumfuata, wakaenda zao.

wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamtazama uso tena. Wakamsindikiza hatta merikebuni.

Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba:

Na kwa sababu bandari haikukaa vema, watu wakae ndani yake wakati wa haridi, walio wengi wakatoa shauri tutweke tukatoke huko illi wapate kufika Foiniki, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi: nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki.

Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Dioskuri.

wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo.

bassi mtu aliye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, illi aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.

na kupita kwenu na kuendelea hatta Umakedoni; na tena toka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Yahudi.

Nitakapomtuma Artema kwako an Tukiko, jitahidi kuja kwangu hatta Nikopoli; maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo