Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 16:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 bassi watiini watu kama hawa, na killa mtu afanyae kazi pamoja nao, na kujitaabisha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumika pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumika pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumika pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 16:16
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nisalimieni Trufina na Trufosa, wenye ijtihadi katika Kristo.


Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,


Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yetu.


Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Staku, mpenzi wangu.


Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.


Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.


mkitumikiana katika khofu ya Kristo.


Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu.


Lakini, ndugu, tunataka mwajue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamieni katika Bwana, na kuwaonyeni;


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni.


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


Bassi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hawo, illi tuwe watendaji wa kazi pamoja na kweli.


tena ulistahimili na kuwa na uvumilivu, na kwa ajili yangu umejitaabisha wala hukuchoka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo