Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 16:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, hakikisheni kwamba hana hofu yoyote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana Isa, kama mimi nifanyavyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, hakikisheni kwamba hana hofu yoyote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana Isa, kama mimi nifanyavyo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 16:10
11 Marejeleo ya Msalaba  

AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.


Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo.


Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


bassi mtu aliye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, illi aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.


Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


illi mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na baja ya cho chote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo