Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 16:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: Fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: Fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyoyaagiza makundi ya waumini ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyowaagiza waumini wa Galatia, fanyeni vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 16:1
20 Marejeleo ya Msalaba  

Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.


Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul.


Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia.


Hatta akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya inchi ya Galatia na Frugia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.


Baada ya miaka mingi nalifika niwaletee watu wa taifa langu sadaka na matoleo.


Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia khabari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemi:


Akampa mkono, akamwinua; hatta akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, yu hayi.


kwa mahitaji ya watakatifu, mkiwashirikisha; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.


mtu akiwa na njaa, ale nyumbani; msipate kukutanika kwa hukumu. Nayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.


Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu),


Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.


na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia,


illa neno moja walitutakia, tuwakumbuke maskini; na neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.


nikisikia khabari ya upendo wako na ya imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote;


Maana tuna furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu lmeburudishwa nawe, ndugu.


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia hii, akamwona ndugu yake yu muhitaji, akamzuilia huruma zake, je! huko ndiko kumpenda Mungu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo