Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 15:58 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

58 Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

58 Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

58 Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

58 Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

58 Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana Isa, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana Isa si bure.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

58 Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana Isa, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana Isa si bure.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 15:58
42 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.


Akamwambia yule nae, Na wewe uwe juu ya miji mitano.


Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:


Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha burre kwenu.


Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.


mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.


Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;


nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre.


Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa, asiutunze uhayi wake; illi kusudi ayatimize yaliyopungua katika khuduma yenu kwangu.


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.


mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu;


mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.


Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida.


ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo