Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 15:57 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

57 Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

57 Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

57 Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

57 Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

57 Lakini Mungu apewe shukrani, yeye atupaye ushindi kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

57 Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 15:57
18 Marejeleo ya Msalaba  

Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Alipokwisha kusema haya akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula.


Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Bassi, kama ni hivi, kwa akili zangu naitumikia sharia ya Mungu, bali kwa mwili sharia ya dhambi.


Lakini katika mambo haya yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.


Angalieni, nawaambieni siri; hatutalala wote, lakini wote tutabadilika,


ninyi nanyi mkisaidiana kwa ajili yetu katika kuomba, illi, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa kazi ya watu wengi, watu wengi watoe mashukuru kwa ajili yetu.


Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.


Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo.


mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo