Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 15:54 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

54 Bassi, uharibifu huu utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

54 Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa; ushindi umekamilika!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

54 Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa; ushindi umekamilika!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

54 Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa; ushindi umekamilika!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

54 Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

54 Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

Tazama sura Nakili

1 Wakorintho 15:54
12 Marejeleo ya Msalaba  

kwa kuwa hawawezi kufa tena, maana huwa sawasawa na malaika; tena ni wana wa Mungu kwa kuwa wana wa ule ufufuo.

wakaubadili utukufu wa Mungu asiye ua uharibifu kwa mfano wa sura ya bin-Adamu aliye ua uharibifu, na ya nyama wenye mbawa, na ya nyama wenye miguu mine, na ya nyama watambaao.

wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;

Bassi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hatta mkazitii tamaa zake;

Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.

Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti.

Kwa maana sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, hali kuvikwa vazi jingine, illi kitu kile kipatwacho na mauti kimezwe na uzima.

atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.

Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.

Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo