Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 15:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mimi niliwakabidhi nyinyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mimi niliwakabidhi nyinyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mimi niliwakabidhi nyinyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama Maandiko yanavyosema,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko,

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 15:3
38 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.


Nae akawaambia, Enyi wapumbavu, na wenye mioyo mizito katika kuyaamini yote waliyoyasema manabii!


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu,


Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.


Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili: Alichukuliwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana kondoo asivyolia mbele yake amkatae manyoya, Vivyo hivyo yeve nae hafunui kinywa chake.


ambae Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa damu yake, kwa njia ya imani, illi aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizotangulia, katika uvumilivu wa Mungu:


aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowakhubirini, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:


Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


MAANA killa Kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wami Adamu amewekwa kwa ajili ya wana Adamu katika mambo yamkhusuyo Mungu, illi atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;


na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo