Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 15:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowakhuhirieni; isipokuwa mliamini burre.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 15:2
31 Marejeleo ya Msalaba  

Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.


wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.


Na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa, akakaa na Filipo: akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.


Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


tena kama Kristo hakufufuliwa, bassi, kukhubiri kwetu ni burre na imani yenu ni burre.


Kwa maana sisi tu manukato va Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


Mmepatikana na mateso makubwa namna hii burre? ikiwa ni burre.


Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu.


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


Yafaa nini, ndugu zangu, mtu akisema ana imani, nae hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?


Vivyo hivyo na imani, isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake.


Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo