Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 14:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Sasa ndugu zangu, nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya, nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 14:6
32 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni.


Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake?


Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.


Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, bali faida yao walio wengi, wapafe kuokolewa.


UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.


Hatta vitu visivyo na uhayi vitoapo sauti, ikiwa filimbi, ikiwa kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?


Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiojua kunena, illakini hii si hali yangu katika ilmu; lakini katika killa neno tumedhihirishwa kwenu.


SINA buddi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia njozi na mafunuo ya Bwana.


Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi.


Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye:


kwa hayo, myasomapo, mtaweza kutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo;


Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo.


Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.


Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,


Killa andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibu katika haki;


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenn tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo