Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 14:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika daraja ya mjinga ataitikaje, Amin, baada ya kushukuru kwako, nae hayajui usemayo?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezaje mtu wa kawaida aliye katika mkutano kuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina”, kama haelewi unachosema?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezaje mtu wa kawaida aliye katika mkutano kuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina”, kama haelewi unachosema?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezaje mtu wa kawaida aliye katika mkutano kuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina”, kama haelewi unachosema?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Ikiwa unabariki kwa roho, mtu mwingine atakayejikuta miongoni mwa hao wasiojua, atawezaje kusema “Amen” katika kushukuru kwako, wakati haelewi unachosema?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Ikiwa unabariki kwa roho, mtu mwingine atakayejikuta miongoni mwa hao wasiojua, atawezaje kusema “Amen” katika kushukuru kwako, wakati haelewi unachosema?

Tazama sura Nakili

1 Wakorintho 14:16
30 Marejeleo ya Msalaba  

akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.

mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.

Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.

Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.

Kuna na mengine mengi aliyoyafanya Yesu, nayo yakiandikwa moja moja, nadhani hatta ulimwengu wote usingetosha kwa vitabu vitakavyoandikwa. Amin.

Wayahudi wakastaajabu, wakinena, Amepataje huyo kujua elimu, nae hajasoma?

Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.

na akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangii.

Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazizai matunda.

Maana yeye anenae kwa lugha, haneni na watu, bali na Mungu; maana hapana asikiae; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amin.

Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.

Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.

Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.

wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo