Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 13:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Bassi, sasa inabaki imani, tumaini, upendo, hizi tatu; na iliyo kuu katika hizi ni upendo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Sasa yanadumu haya matatu: Imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Sasa yanadumu haya matatu: Imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 13:13
43 Marejeleo ya Msalaba  

Nae akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.


lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.


Mambo yenu yote yatendeke katika upendo.


Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.


NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga.


Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejuliwa nae.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


tena alikufa kwa ajili ya wote, illi walio hayi wasiwe hayi kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu.


Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki:


Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi.


Bassi msiutupe njasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.


Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;


tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia,


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.


Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.


Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.


Na killa mwenye kunitumainia hivi hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.


Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo