Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 13:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NIJAPOSEMA kwa lugha za wana Adamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upato uvumao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Hata kama nikisema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolia au toazi linalovuma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 13:1
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atawajibu, akinena, Amin, nawaambieni, Kadiri msivyomtendea mmojawapo katika hawo walio wadogo, na mimi hamkunitendea.


Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya;


Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambae Kristo alikufa kwa ajili yake.


na mwingine kutenda kazi za miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;


Na sikio likisema, Mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! si wa mwili kwa sababu hiyo?


Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, ipendavyo Roho yule yule;


Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.


Maana yeye anenae kwa lugha, haneni na watu, bali na Mungu; maana hapana asikiae; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.


Anenae kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali akhutubuye hulijenga Kanisa.


Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa.


NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga.


ya kuwa alichukuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwana Adamu ayanene.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki:


zaidi ya yote mwe na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husetiri wingi wa dhambi;


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama santi ya maji mengi na kama sauti ya radi kuu. Nikasikia sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo