Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 12:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Mungu ameweka katika kanisa: Kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Mungu ameweka katika kanisa: Kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Mungu ameweka katika jumuiya ya waumini kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, na aina mbalimbali za lugha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Mungu ameweka katika jumuiya ya waumini kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 12:28
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya;


Simon ambae alimpa jina la pili Petro, na Andrea, ndugu yake; Yakobo na Yohana, Filipo na Bartholomayo.


Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yemsalemi hatta Antiokia.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunaui wala Kanisa la Mungu:


Bali Mungu amevitia viungo killa kimoja katika mwili kama alivyotaka.


Je! wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanatenda miujiza?


wote wana karama za kuponya wagonjwa? wote wanena lugha? wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo njema zaidi.


Maana yeye anenae kwa lugha, haneni na watu, bali na Mungu; maana hapana asikiae; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.


Anenae kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali akhutubuye hulijenga Kanisa.


Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa.


mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;


ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho;


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo