Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 12:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Bali Mungu amevitia viungo killa kimoja katika mwili kama alivyotaka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 12:18
18 Marejeleo ya Msalaba  

Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.


Bassi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;


lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye.


Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? kama wote ni sikio ku wapi kuona?


Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?


Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; hali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima kile kiungo kilichopungukiwa;


Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.


lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na killa mbegu mwili wake.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,


akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,


Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo