Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 12:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa maana katika Roho mmoja wa Mungu wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 12:13
36 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu.


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa mataifa pia? Naam, wa mataifa pia;


Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;


wote wakabatizwa kwa Musa katika wingu na katika bahari;


Lakini kabla ya kuja imani tulikuwa tumewekwa chini ya sharia, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili;


Bwana mmoja, imani moja, ubatizo umoja,


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru.


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo