Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 12:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 12:11
18 Marejeleo ya Msalaba  

Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako.


Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu nipendavyo? Au jicho lako ni ovn kwa sababu ya kuwa mimi mwema?


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


Upepo huenda utakako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na killa mtu aliyezaliwa kwa Roho.


Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao.


Bassi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;


Bassi, kama ni hivyo, atakae (kumrehemu) humrehemu, na atakae kumfanya mgumu humfanya mgumu.


Bali Mungu amevitia viungo killa kimoja katika mwili kama alivyotaka.


Pana tofauti za karama; bali Roho yule yule.


pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu yule yule azitendae kazi zote katika wote.


Lakini Mungu alivyomgawia killa mtu—kama Mungu alivyomwita killa mtu, na aenende vivyo hivyo. Na ndivyo ninavyoagiza katika Makanisa yote.


Maana nipendalo ni watu wote wawe kama mimi nilivyo; illakini killa mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.


Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya cheo tulichopimiwa na Mungu, yaani kadiri ya kufika hatta kwenu.


ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;


Lakini killa mmoja wetu alipewa neema, kwa kadiri ya kipawa cha Kristo.


Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo