Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 11:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, tusipate kupasishwa adhabu pamoja na dunia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Tunapohukumiwa na Bwana Isa, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Tunapohukumiwa na Bwana Isa, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 11:32
22 Marejeleo ya Msalaba  

Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyekosa si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali kipawa cha neema kilikuja kwa ajili ya makosa mengi, kikaleta kuachiliwa.


Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa dunia bii? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia liii kuwa upumbavu?


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.


Lakini tukijihukumu vema nafsi zetu, tusingehukumiwa.


Bassi, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojane;


Katika hao wamo Humenayo na Iskander, ambao nimempa Shetani wafundishwe wasimtukane Mungu.


Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.


Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo