Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 11:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Maana killa mwulapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hatta ajapo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana Isa hadi ajapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana Isa mpaka ajapo.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 11:26
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi nikishika njia kwenda kuwaandalia mahali, nitakuja tena, niwakaribisheni kwangu; illi nilipo mimi, nanyi mwepo.


Yesu akamwambia, Nikitaka huyu akae hatta nijapo imekukhusu nini? wewe unifuate mimi.


Bassi neno hili lilienea katika ndugu kwamba mwanafunzi yule hafi: walakini Yesu hakumwambia, Hafi; bali, Nikitaka akae hatta nijapo imekukhusu nini?


wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.


Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza;


atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.


Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake.


Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake,


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo