Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 1:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Yeye atawaimarisheni nyinyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Yeye atawaimarisheni nyinyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Yeye atawaimarisheni nyinyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Atawafanya imara hadi mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 1:8
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hatta upande huu chini ya mbingu, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa katika siku yake.


Kadhalika itakuwa katika siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.


Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi siku ile watakayofunuliwa wanawa Mungu.


kazi ya killa mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto utajaribu kazi ya killa mtu, ni wa namna gani.


kumtolea Shetani mtu huyo, mwili uadhibiwe, illi roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.


Maana hatuwaandikii ninyi neno, illa yale msomayo, au kuyakiri; nami nataraja ya kuwa mtayakiri hatta mwisho;


vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.


Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,


apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa.


mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,


niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo;


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku.


msifadhaishwe upesi na kuaeha nia yenu, wala msistushwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, ya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.


Lakini Bwana ni mwaminifu, atakaewafanyeni imara na kuwaokoeni na yule mwovu.


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo