Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 1:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Lakini sisi tunamhubiri Al-Masihi aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Lakini sisi tunamhubiri Al-Masihi aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 1:23
22 Marejeleo ya Msalaba  

Na yu kheri ye yote asiyechukiwa nami.


Wakachukizwa nae. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika inchi yake mwenyewe, na nyumbani mwake mwenyewe.


Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;


Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


nae alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, na vitu ambavyo haviko, illi avibatilishe vilivyoko;


Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.


Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa.


Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.


Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.


ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?


Na mimi, ndugu, ikiwa ninakhubiri khabari ya kutahiriwa, mbona ningali nikiudhiwa? Hapo kwazo la msaiaba limebatilika.


Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo