Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 1:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Kwa kuwa katika hekima ya Mungu ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mwenyezi Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 1:21
28 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu him atatupwa nje.


Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa;


Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hatta kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake hazitafutikani!


Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


bali kwao waitwao, Wayahudi na Wayunani pia, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.


Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wana Adamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wana Adamu.


bali Mungu aliyachagua mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena alivichagua vitu dhaifu vya dunia illi wenye nguvu waaibishwe;


Tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, tusipate kupasishwa adhabu pamoja na dunia.


Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.


Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.


Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! hamstahili kuhukumu hukumu zilizo ndogo?


Lakini Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,


Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkujua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.


akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,


illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni;


Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae,


Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.


Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa.


ajue va kuwa veve amrejezae mwenye dhambi, atoke katika njia ya upotovu, ataiokoa roho ya mtu yule na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo