Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 1:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu, ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu, ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu, ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 1:18
21 Marejeleo ya Msalaba  

Tazameni, enyi mnaodharau, kjitaajabuni, katowekeni; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi msiyoisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.


Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.


Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.


wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowakhuhirieni; isipokuwa mliamini burre.


Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.


Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa.


Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao.


Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.


maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;


Ijapokuwa injili yetu imesetirika, imesetirika kwao wanaopotea;


kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.


na katika madanganya yote ya udhalimu kwao wanaopotea: kwa sababu hawakukubali kuipenda kweli, wapate kuokolewa.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo