Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 1:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Bassi, nasema neno hili, ya kwamba killa mtu wa kwenu husema, Mimi wa Paolo, na mimi wa Apollo, na mimi wa Kefa, na mimi wa Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Nataka kusema hivi: Kila mmoja anasema chake: Mmoja husema, “Mimi ni wa Paulo”, mwingine: “Mimi ni wa Apolo”, mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni wa Kristo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Nataka kusema hivi: Kila mmoja anasema chake: Mmoja husema, “Mimi ni wa Paulo”, mwingine: “Mimi ni wa Apolo”, mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni wa Kristo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema, “Mimi ni wa Paulo”, mwingine: “Mimi ni wa Apolo”, mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni wa Kristo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa”; na mwingine, “Mimi ni wa Al-Masihi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Al-Masihi.”

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 1:12
20 Marejeleo ya Msalaba  

Bali ninyi nisiitwe Rabbi; maana mwalimu wenu yu mmoja ndiye Kristo, na ninyi nyote ni ndugu.


Akampeleka kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, Wewe Simon, mwana wa Yona, utakwitwa Kefa (tafsiri yake, Petro).


Bassi Myahudi mmoja, jina lake Apollo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akalika Efeso; nae alikuwa hodari wa maandiko.


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Kwa maana nimearifiwa khabari zenu, ndugu, na wale walio wa nyumba ya Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.


na ya kuwa alionekana na Kefa; tena na wathenashara;


Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.


Lakini kwa khabari za Apollo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja nao ndugu, nae hakupenda kabisa kwenda sasa; lakini atakwenda sitakupopata nafasi.


Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.


Lakini, nasema hivi, ndugu, muda ubakio si mwingi; bassi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;


Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?


Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.


Lakini nasema neno liili, Apandae haha atavuna haha; apandae kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


Nisemayo ni haya; agano lililofanywa imara kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka aruba mia na thelathini baadae hailitangui, hatta kuibatilisha abadi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo