Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wakorintho 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Al-Masihi Isa, na Sosthene ndugu yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuwa mtume wa Al-Masihi Isa, na Sosthene ndugu yetu.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 1:1
28 Marejeleo ya Msalaba  

Ulipokuwa mchana akawaita wanafunzi wake: akachagua watu thenashara miongoni mwao, ambao aliwaita mitume.


Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.


Bassi Yesu akawaambia marra ya pili, Amani kwenu; kama Baba alivyonipeleka, nami nawatuma ninyi.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu:


Na Wayunani wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sunagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Na Gallio hakuyaona mambo hayo kuwa kitu.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


nikiomba nije kwenu sasa katika siku hizi hizi, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu:


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Maana mimi mdogo katika mitume, nisiyestahili kutajwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.


Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa kitu walicho nacho mitume walio wakuu.


Maana ishara za mtume zilitendwa kati yenu katika uvumilivu wote, kwa ishara na maajabu na nguvu.


Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini, bali kwanza walijitoa nafsi zao, wakampa Bwana; kiisha wakatupa sisi pia, kwa mapenzi ya Mungu,


PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu;


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo