Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 6:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Na wale walio na mabwana waaminio, wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; hali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya kazi zao wamekuwa wenye imani na kupendwa. Uwafundishe mambo haya, na kuonya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Watumwa ambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharau kwani ni ndugu zao. Badala yake, wanapaswa kuwatumikia hata vizuri zaidi, maana hao wanaopata faida kutokana na kazi yao ni waumini ambao wanawapenda. Unapaswa kufundisha na kuhubiri mambo haya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Watumwa ambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharau kwani ni ndugu zao. Badala yake, wanapaswa kuwatumikia hata vizuri zaidi, maana hao wanaopata faida kutokana na kazi yao ni waumini ambao wanawapenda. Unapaswa kufundisha na kuhubiri mambo haya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Watumwa ambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharau kwani ni ndugu zao. Badala yake, wanapaswa kuwatumikia hata vizuri zaidi, maana hao wanaopata faida kutokana na kazi yao ni waumini ambao wanawapenda. Unapaswa kufundisha na kuhubiri mambo haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Wale watumwa ambao wana mabwana waaminio, haiwapasi kupunguza heshima yao kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie hata vizuri zaidi, kwa sababu wale wanaonufaika na huduma yao ni waumini, ambao ni wapendwa wao. Fundisha mambo haya na uwahimize kuyafuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wale watumwa ambao wana mabwana waaminio, haiwapasi kupunguza heshima yao kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie hata vizuri zaidi, kwa sababu wale wanaonufaika na huduma yao ni waaminio, ambao ni wapenzi wao. Fundisha mambo haya na uwahimize kuyafuata.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 6:2
31 Marejeleo ya Msalaba  

Bali ninyi nisiitwe Rabbi; maana mwalimu wenu yu mmoja ndiye Kristo, na ninyi nyote ni ndugu.


Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Lakini iwapo matawi mengine yamekatiwa, na wewe mzeituni mwitu ulitiwa kati yao ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,


Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, illi awe mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu;


Kwa sababu hiyo na mimi, tangu nilipopata khabari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,


ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili;


kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


NINYI bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


Uwaagize watu hayo na kuwafundisha hayo.


USIMKEMEE mzee, bali mwonye kama baba, na wadogo wako kama ndugu:


BALI wewe nena mambo yapasayo mafundisho ya uzima,


Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.


Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae;


na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu;


Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, hutukana matukufu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo