Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 6:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 yeye pekee aishiye milele, anayedumu katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 6:16
30 Marejeleo ya Msalaba  

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Yesu akamwambia, Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba?


Si kwamba mtu amemwona Baba, illa yeye atokae kwa Mungu huyu ndiye aliyemwona Baba.


Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Kabla Ibrahimu hajakuwapo, Mimi nipo.


kwake yeye utukufu katika Kanisa, na katika Kristo Yesu hatta vizazi vyote vya milele na milele. Amin.


Sasa Mungu, Baba yetu, atukuzwe milele na milele. Amin.


nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Na hii ndiyo khabari tuliyoisikia kwake, na kuikhubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza yo yote hamna ndani yake.


bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


Nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wana Adamu, nae atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Mungu wao.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.


wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo